Usugu wa dawa kumaliza watu
ULAYA : Utafiti unaonyesha zaidi ya watu milioni 39 wanaweza kupoteza maisha kutokana na usugu wa dawa za antibayotiki zinazotibu maambukizi kati ya sasa na mwaka 2050.
Ripoti inaonyesha kuwa watu milioni 1.91 wako hatarini kupoteza maisha ifikapo mwaka 2050 ikiwa ni ongezeko la asilimia 70 kwa mwaka ukilinganishwa na mwaka 2022.
Huku zaidi ya watu milioni 1 wamepoteza maisha duniani kuanzia mwaka 1990 hadi 2021.
Kutokana na tatizo hili,wataalamu wa afya duniani wametoa tahadhari ya kuanza kuchukua hatua ya kulinda watu.
Unaambiwa ongezeko hili linaweza kuongezeka kwenye mifumo ya afya na uchumi wa mataifa na kupoteza pato la taifa la kati kwa mwaka ambapo ni sawa na dola trilioni moja hadi 3.4 ifikapo 2030.
SOMA : Matumizi holela ya dawa sababu usugu wa tiba