Utaratibu biashara pembezoni mwa barabara waelezwa

DODOMA; SERIKALI imesema imeweka utaratibu kwa ajili ya wafanyabiashara wenye nia ya kutumia maeneo yaliyopo pembezoni mwa barabara.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya ametoa kauli hiyo leo Februari 5, 2026, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga aliyeuliza utaratibu gani wananchi wafuate wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara za TANROADS hususan maeneo ya Mkambe, Kidatu na Mkula.

“Kwa mujibu wa marekebisho ya Kanuni za Matumizi ya Barabara za Mwaka 2025, Kanuni ya 36(4) imeweka utaratibu kwa ajili ya wafanyabiashara wenye nia ya kutumia maeneo yaliyopo pembezoni mwa barabara.

“Kanuni zinaelekeza kuwa, mfanyabiashara anayetaka kupanga katika hifadhi ya barabara atajaza fomu maalumu ya maombi inayotolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na atatakiwa kulipa ada ya maombi kabla ya kuwasilisha fomu hiyo.

“Wakala baada ya kupokea maombi hayo itayachakata na yale yatakayokidhi vigezo, TANROADS itatoa kibali na kumjulisha mwombaji gharama atakazopaswa kulipia kwa mujibu wa sheria,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button