DAR ES SALAAM: WATANZANIA wameshauriwa kuchukua tahadhari za kifedha kwa ajili ya dharura za kibinadamu na matumizi ya baadaye.
Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja (UTT AMIS) leo Machi 6, 2025 imetoa elimu kuhusu umuhimu wa uwekezaji wa fedha kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), hususan wanawake katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Tazara jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Ofisa Masoko na Mahusiano kwa Umma UTT AMIS, Medson Enock amesema lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwawezesha wanawake kutambua umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
“Lengo letu kubwa ni kuwafahamisha watu umuhimu wa kujiwekea akiba, hasa akiba ya kifedha. Akiba si kwa ajili ya mtu binafsi tu, bali pia kwa jamii inayomzunguka. Katika hali ya dharura, mtu anayejua kuweka akiba anaweza kujisaidia yeye mwenyewe au kusaidia wengine,” amesema Enock.
SOMA ZAIDI: Serikali yawashauri wazazi kufundisha watoto kujiwekea akiba
Kwa upande wake, Ofisa Rasilimali Watu wa TSN, Catherine Chamungwana, amesema taasisi yao iliona ni vyema kuwapatia wafanyakazi mafunzo kuhusu uwekezaji, kwani wengi wao hususan wanawake wanapokea mishahara lakini hawaweki akiba wala kuwekeza.
“Wanawake wengi tunafanya kazi na kutumia muda mwingi ofisini. Tunapokea mishahara, lakini mara nyingi hatuwekezi, tunatumia fedha bila mpangilio wa baadaye. Hivyo, tuliona ni muhimu kupata nafasi ya kujifunza kuhusu uwekezaji, na sasa tumepata uelewa wa kuweka fedha katika mifuko mbalimbali,” amesema Catherine.
Glory Munisi, ambaye ni Mkaguzi wa Maandishi katika TSN na mmoja wa waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo, alisema amejifunza mengi, ikiwemo umuhimu wa kuandaa maisha ya baadaye kwa kuwekeza mapema.
“Nimejifunza jinsi ya kuilinda kesho yangu baada ya kustaafu au iwapo nitakumbwa na dharura inayohitaji utatuzi wa haraka,” amesema Glory.
Washiriki waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo wametoa wito kwa wananchi wote, hususan vijana, kuanza kuwekeza mapema na pia kuwawekezea watoto wao, kwani hatua hiyo itawasaidia katika maisha yao ya baadaye.
I was BROKE and desperate… now I make $3,000+ weekly from my couch! Just 30 days ago, I was stuck in a dead-end job, living paycheck to paycheck. Then I found this secret method—and everything changed Anyone can do this in their free time. Spots are LIMITED! Don’t miss out!
Join now➤➤ http://Www.WorksProfit7.Com