UWAA yashauriwa kuchangamkia fursa utalii

ARUSHA: Meya wa Jiji la Arusha, Maxmillan Iraghye ameutaka Umoja wa Washereheshaji Mkoa wa Arusha (UWAA) kuchangamkia fursa za utalii zilizopo mkoani.

Pia ameutaka umoja huo kuacha kujikita katika kusherehesha harusi na ubarikio kwa kufanya hivyo ni kujirudisha nyuma katika maendeleo ya karne hii ya sayansi na teknolojia.

Iraghye alisema hayo Machi 13 katika Iftar iliyoandaliwa na UWAA na kushirikisha viongozi wa dini na mbalimbali na serikali lengo umoja huo ni kuwaunganisha watanzania kuwa na umoja ,mshikamano na upendo bila kujali dini,itikadi na kabila kwani wote ni watanzania na wanajenga nyumba moja haina haja ya kugombana.

Meya alisema Mkoa wa Arusha una fursa nyingi ikiwemo utalii wa safari, mikutano, michezo na matibabu vyote vinahitaji washereheshaji lakini baadhi yenu mmejikitaka katika sehemu moja wakati mnauwezo wa kuzifanya kazi zote hivyo ni wakati wa kujitoa na kushiriki katika utalii wa mikutano na kuzifanya kazi hizo bila kuwa na uoga.

Alisema inasikitisha kuona katika utalii wa mikutano AICC, Grand Melia Mount Meru Hotel na Ngurdoto Hotel na kwenye mikutano ya siasa na sehemu nyingine washereheshaji wanatoka mikoa mingine ama nje ya nchi wakati mko hapa na mnasifa zote za kuizifanya kazi hizo ifike sasa mbadilike na kujikita huko bila ya uoga.

Mstahiki Meya huyo aliendelea kusema kuwa washereheshaji wanapaswa kujianda kwani Jiji la Arusha ni Jiji la Utalii wa aina hizo nne na mwakani zitakuwa na fursa nyingi hivyo aliwaasa kujiendeleza zaidi na kujua lugha za kimataifa zaidi ya nne ili waweze kupata fursa hizo za kuwapokea wageni na kupata ajira.

‘’Ni wakati wa UWAA kutoa katika kusherehesha harusi na ubarikio na kujikita katika fursa za utalii kwani Arusha baadae inawahitaji sana vinginevyo kazi hizo zitafanywa na wengine kutoka nje kitu ambacho sio sawa,” alisema.

Aidha, aliwataka UWAA kuwa wamoja na kupendana lengo ni kutaka wote kupeana kazi na kuacha kung’ang’ania kazi zote kwa kufanya hivyo ni uchoyo kitu ambacho hakipendezi kwani IFTAR iliyoandaliwa ionyeshe upendo wa dhati kwa jumuiya hiyo.

Naye Mwenyekiti wa UWAA Mkoa wa Arusha,Mohamed Msofe alisema lengo la IFTAR iliyoandaliwa na umoja huo ni kutaka kuwaunganisha watanzania wote kuwa wamoja na kupendana na kuacha kuishi kwa chuki ,fitina,uhasama na uaduni kwani sio mila na destuli za mtanzania na kusema kuwa wote wanajenga nyumba moja.

Msofe alisema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwaunganisha watanzania wote bila kujali dini,kabila na itikadi na kuwa wamoja kwa kushirikiana kwa hali na mali hivyo usia huo unapaswa kuendelezwa na kamwe wasikubali kutenganishwa kwa maslahi ya wengine.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa dini zote Shekh Twaha Muhammad Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mariadhiano na Amani Tanzania Jiji la Arusha alisema nchi inahitaji amani na upendo hivyo kila mmoja afanya hivyo kwa maslahi ya nchi na ameupongeza UWAA kwa kufuturisha waislamu na wakristu kwani wote wako katika mfungo wa Ramadhani na Kwaresma.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button