Vazi la Kaptula linampendeza kila mtu

KAPTULA ni  vazi linalovaliwa na wanawake na wanaume juu ya eneo la nyonga yao.likizunguka kiuno na kugawanyika ili kufikia sehemu ya juu ya miguuni, wakati mwingine hupanda magotini lakini si kufunika urefu mzima wa miguuni.

Ni toleo la kufupishwa kwa suruali ambalo ufunika mguu mzima ndio sababu kwa kingereza huitwa (short pens) kwa kuwa linafanana na suruali fupi huku tofauti ikiwa inaanzia kwenye kiuno hadi magotini.

Kwa kawaida Kaptula huvaliwa katika hali ya hewani ya joto au katika mazingira ya faragha na mtiririko wa hewani muhimu kuliko ulinzi wa miguuni.

Advertisement

Katika jamii nyingi za Afrika vazi la Kaptula ni lawavulana wadogo huku wakubwa wao na wazee wakiwa wanavaa suruali ndefu. SOMA: Malika Designer abuni mavazi kwa viongozi

Nchi za Amerika na uingereza pia zilikuwa na mitindo hii y kuwapa  wavulana Kaptula huku wakipewa suruali ndefu walipokomaa.

Haya yalifanyika katika Karne ya 18 lakini kwa sasa vazi hili limekuwa la wote.Kaptula pia hutumika sana kwenye michezo ambapo wanaspoti huvalia vazi hili maana limwezesha kucheza bila kuhisi kubanwa na kuwa huru na vazi hilo.

Hata hivyo vazi hili Lina sehemu maalumu ya kuvaa, kwa wafanyakazi au Baadhi ya maeneo kama sehemu ya ibada, harusini kaptura haifai. Katika ulimwengu wa mitindo, Kaptula hazivaliwi tu nyumbani bali hata baharini au club.

Licha ya kuwa vizuri kuvaa Kaptula ambazo sasa zinakuja na mitindo na vifaa mbalimbali hukuruhusu kuonekana maridadi bila kuwa na Fujo.

Wanawake wengi huvaa suruali fupi kama mavazi ya nyumbani lakini sasa wengine pia huvaa kama vazi wakati wa kusafiri au katika hafla rasmi.

Kuna aina nyingi za Kaptula za wanawake kwenye soko kama vile kaptura za denim, hot panis, overalls fupi kifupi cha pamba za zaidi. Zipo pia Kaptula za vitambaa kama vile vya polka dot au mauwa mauwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *