TETESI za usajili zinasema mshambuliaji Victor Osimhen anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 75 amekataa ofa ya Manchester United kujiunga na timu hiyo kujaribu kumaliza mkataba wake wa mkopo Galatasaray. (Heber Sarikirmizi – Turkey)
Marcus Rashford hajafutilia mbali uwezekano wa kujiunga na West Ham United kwa mkopo iwapo uhamisho kwenda Borussia Dortmund au AC Milan hautafanikiwa. (GIVEMESPORT)
AC Milan imeacha mpango wa kumsajili Rashford na badala yake inaupa kipaumbele usajili wa beki wa kulia wa Manchester City, Kyle Walker. (L’Equipe – France)
Liverpool inajiandaa kuwatoa Federico Chiesa, Wataru Endo na Harvey Elliott kwa Real Sociedad katika jitihada za kupunguza gharama ya kumsajili nyota wa Kijapani, Takefusa Kubo anayeonaekana kufaa kuchukua nafasi ya Mohamed Salah. (El Nacional – Spain)
Al Hilal ya Saudi Arabia inakaribia kuwasajili Mohamed Salah na Virgil van Dijk, ambao wote wawili watajiunga na timu hiyo kutoka Liverpool kwa uhamisho huru. (Fichajes – Spain)
Chelsea inatumaini kujadili ada ya chini na Crystal Palace kwa ajili ya Marc Guehi anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Mail Sport)
Beki huyo wa zamani wa The Blues amebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake. (Mail Sport)