Vijana 1,000 wameajiriwa SinoTan Park -Msigwa

PWANI: MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema vijana zaidi ya 1,000 wameajiriwa katika kiwanda cha SinoTan Park kilichopo Kibaha, mkoani Pwani, kianchozalisha bidhaa mbalimbali kama majokofu, nguo, na vifaa vingine.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Machi 16, eneo la Bandari ya Kwala, Msigwa amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inaendelea kuimarisha miradi ya viwanda na bandari, ambapo tayari kontena zaidi ya 700 zimepokelewa bandarini hapo.

Ameeleza kuwa sekta ya viwanda imeleta mapinduzi chanya ya kiuchumi, huku mapato yake yakifikia Sh trilioni 2 katika miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Aidha, ajira zaidi ya laki tano zimeongezeka kupitia miradi mbalimbali ya viwanda.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button