Vijana 600,000 waajiriwa Jamukaya

VIJANA wapatao 600,000 kutoka Kanda ya Ziwa wamepata fursa za ajira katika kampuni ya Jambo Food Product ‘Jamukaya’ iliyopo kata ya Ibadakuli mkoani Shinyanga.

Hatua hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira.

Meneja wa kampuni hiyo, Nickson George ametoa takwimu hizo wakati wa hafla ya kuboresha bidhaa zao mbalimbali zinazozalishwa kwenye kiwanda hicho.

George amesema wao kama sekta binafsi kampuni imejizatiti kutoa ajira za kudumu 400,000 ukijumlisha na wale wa ajira ya muda mfupi wanakuwa 600,000 hivyo kila siku watu hao wako kazini na serikali inapata mapato yake.

“Tumeamua kubadilisha muonekana wa sura ya mpya ya bidhaa baada ya kampuni kufikisha miaka 20 ya uzalishaji wa bidhaa zake hivyo tumeheshimu wateja wetu,” amesema George.

George amesema mteja akiona muonekano mpya asiwe na mashaka kwani kuna usemi unaoeleza ‘Hawa ndio sisi’ ikimaanisha muonekano huo usiwape wasiwasi bali ni kampuni hiyo hiyo ikiendelea kuwapa furaha wateja wake.

SOMA: Wanaotafuta ajira serikalini waongezeka – Ripoti

Habari Zifananazo

Back to top button