Vijana wapewa mwelekeo mpya mashindano ya sheria

DAR ES SALAAM: Katika zama ambazo jamii inahitaji viongozi wenye maono, vijana wenye ujasiri, na watetezi wa haki zenye mwelekeo wa kijamii, toleo la tano la shindano ya Victory Attorneys National Moot Court Competition (VAC Moot 2025) limeonesha taswira mpya ya kizazi kinachoinuka kwa ari na uzalendo.
Mashindan haya, yaliyoandaliwa na Victors Hub Limited kwa ushirikiano na Chama cha Wanasheria Vijana (AYL-TLS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serengeti Bytes, yamefanyika katika jengo la TLS–Wakili House jijini Dar es Salaam yakibeba kaulimbiu yenye uzito wa kijamii: “Ushuru wa Mali za Kidijitali nchini Tanzania.”
Zaidi ya kuwa jukwaa la kisheria, mashindano haya yamekuwa darasa la maisha mahali ambapo vijana wa Kitanzania wanajifunza kujenga hoja zenye maadili, kufanya kazi kwa timu, kuheshimu tofauti za mawazo na kuamini katika uwezo wao.
“Tumejifunza zaidi ya sheria. Tumejifunza kuwasiliana, kushirikiana, na kusikiliza hoja za wengine kwa heshima,” alisema mmoja wa washiriki kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Victors Hub Limited, Rayson Elijah Luka, alisema kuwa ndoto ya kuanzisha mashindano hayo ilitokana na hamu ya kuona vijana wakitumia taaluma yao kama nyenzo ya kujenga jamii yenye haki, usawa na uwajibikaji.
“Tulitaka kuunda jukwaa linalowezesha vijana kujifunza kutumia maarifa yao kwa manufaa ya watu, si kwa maneno pekee bali kwa vitendo. Leo tunashuhudia ndoto hiyo ikikua,” alisema Luka.
Katika kipindi cha miaka mitano, mashindano hayo yamefikia zaidi ya wanafunzi 1,000 kutoka vyuo vikuu mbalimbali, wakiwemo wale waliopata ajira katika taasisi za kisheria, kampuni binafsi na taasisi za umma. Wengine wameanzisha taasisi ndogo za msaada wa kisheria kwa jamii vijijini.
Wakili Emmanuel Phalet Ukashu, Mwenyekiti wa AYL–TLS, alisema kuwa mashindano hayo yanajenga si tu uelewa wa kisheria, bali pia moyo wa kujitolea kwa jamii.
“Tunawalea wanasheria vijana wenye moyo wa kujituma na kuwasaidia wengine. Sheria si maneno tu, ni chombo cha kubadilisha maisha ya watu,” alisema Ukashu.
Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa TRA, Ted Silkuwasha, alisisitiza umuhimu wa elimu kama kichocheo cha mabadiliko ya kijamii.
“Mageuzi ya kiuchumi na kijamii hayawezi kufanikiwa bila vijana wenye uelewa wa sheria, maadili, na dhamira ya kulinda maslahi ya taifa,” alisema.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com