Viongozi, Wafanyabiashara Afrika kukutana Ghana

Viongozi Afrika kukutana Ghana

VIONGOZI wa Kiserikali na Wafanyabiashara mashuhuri barani Afrika wanatarajia kukutana kwa siku tatu nchini Ghana mwishoni mwa mwezi huu kujadili na kuunda jukwaa la kila mwaka la kiuchumi.

Ofisi ya Rais wa Ghana, Nana Addo Akufo-Addo na ile ya Katibu Mkuu wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA), Wamkele Mene imethibitisha.

Advertisement

 

Mkutano huo uliopangwa kufanyika Jan. 26 hadi 28 mwaka huu utakuwa mkutano wa kwanza wa msururu wa mazungumzo na Mpango wa Mtandao na Mustakabali wa Afrika (APN).

“Mkutano huu utawaleta pamoja viongozi wa kisiasa na kibiashara barani Afrika, pamoja na viongozi wengine wenye mawazo kuhusu Afrika, kujadiliana kuhusu mradi muhimu wa soko moja la Afrika, lakini pia kuunda jukwaa la kila mwaka kwa viongozi wa bara hilo ili kuongoza utekelezaji shirikishi wa Mkataba wa Biashara Huria wa Bara la Afrika ambao ni muhimu sana,” taarifa ya Katibu Mkuu AfCFTA imesema.