Vipaumbele vitano Mpango wa Maendeleo wa Taifa

DODOMA; WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewasilisha bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, ukiwa na vipaumbele vitano.
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi, Kuimarisha uwezo wa Uzalishaji wa Bidhaa Viwandani na Utoaji Huduma, Kukuza Uwekezaji na Biashara, Kuchochea Maendeleo ya Watu na Kuendeleza Rasilimali Watu.