Vishoka tiba asili waonywa matangazo mitandaoni

DAR ES SALAAM:Vishoka wa tiba asili wanaotumia mitandao ya kijamii kutangaza wameonywa kuacha tabia hiyo mara moja na kufata taratibu za usajili uliowekwa na wizara ya Afya.

Mkurugenzi Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dk Paschal Rugajo ametoa onyo hilo kwa waganga wa tiba asili ambapo amesema hatua hiyo ni uvunjifu za sheria.

Asilimia 60 ya watanzania wanatumia tiba asili kabla ya kwenda hospitali huku idadi ya waganga wa tiba asili waliosajiliwa ni 4000 ambapo wengine 7500 hawajasajiliwa bado.

Advertisement

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya tiba asili ya Mwafrika yalioyoambatana na maonesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja alisema hatua muhimu za usajili zinapaswa kufuatwa ili kuhakiki usalama na ubora wa dawa hizo.

“Maadhimisho wiki ya tiba asili ya mwafrika ambapo maonesho yamefanyika kwa mafanikio makubwa na tumetumia fursa hii kuonesha namna serikali ilivyojipanga katika kuhakikisha tiba asili zinafanyika katika mwanga,usalama,ubora na tija.

“Kadiri muda unavyokwenda tunapata waganga wengi wanaosajili lakini pia wanazidi kutambua taratibu na
dawa nyingi zimefanyiwa utafiti ndio sababu serikali imejiamini na kuona huu ni muda muafaka wa zile dawa zilizothibitishwa zinajumuishwa katika hospitali zetu.

Ameeleza kuwa hadi sasa Hospitali saba za rufaa za mikoa zimejumisha tiba asili za dawa ambapo mgonjwa baada ya kuchunguzwa kitaalamu atachagua dawa za asili au za kizungu .

Kwa upande wake Meneja maabara ya chakula na Dawa katika Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Dk Shimo Peter amesema katika taratibu za kusajili sehemu muhimu ni kufanya usajili ili kujua ubora na usalama wa dawa kabla maamuzi yoyote hayajafanyika.

 

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *