CONGO : WAASI wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, wametangaza usitishaji wa mapigano kuanzia leo katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa lengo la kuruhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Tangazo hili linakuja kufuatia wito wa kimataifa wa kuanzishwa kwa njia salama za usafirishaji wa misaada kwa maelfu ya watu waliokosa makao kutokana na vita vinavyoendelea.
Kwa mujibu wa Shirika la Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) limesema kuwa idadi ya vifo iliyoripotiwa na WHO haitaajumuisha miili ya watu waliouawa na mapigano na ambao bado wanapatikana katika vyumba vya kuhifadhia maiti huku miili mingine ikitapakaa mitaani katika mji wa Goma..
Hatahivyo, ripoti ya WHO inasema kuwa, kulingana na mamlaka za mji wa Goma, watu 2,900 wamejeruhiwa kutokana na mapigano hayo.
Wakatihuohuo, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi pamoja na Rais wa Rwanda wamethibitisha kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya SADC unaotarajiwa kufanyika wiki hii. Rais William Ruto wa Kenya unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki.
Mji wa Goma, wenye idadi ya watu milioni 2, uko katikati ya eneo lenye utajiri wa madini na bado upo chini ya udhibiti wa waasi wa M23, ambao wameripotiwa kusonga mbele na kuchukua udhibiti wa maeneo mengine ya mashariki mwa Congo.
SOMA: Jeshi la Congo, Burundi wazuia M23 kuingia Bukavu