Wabunge wakagua miundombinu upokeaji mafuta

KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imetembelea mkoani hapa kwa ajili ya kuangalia miundombinu ya upokeaji wa mafuta na ile ya kuhifadhia nishati hiyo.

Wabunge hao walipata fursa ya kutembelea Bandari ya Mtwara, katika sehemu ambayo meli inafunga gati kwa ajili ya kushusha mafuta na ile inayotoa mafuta kupeleka kwenye hufadhi za mafuta mkoani hapa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja Nchini (PBPA), Erasto Mulokozi amesema, mkoa huo kuna hifadhi mbili za mafuta za zenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 40.

Habari Zifananazo

Back to top button