Wachezaji 500 vishale kuvaana Arusha

DAR ES SALAAM; WACHEZAJI 500 kutoka nchi za Afrika Mashariki wanatarajia kukutana katika michuano miwili ya wazi ngazi ya klabu na taifa itakayofanyika kuanzia Juni 27, mwaka huu mkoani Arusha.

Katibu Mkuu wa Chama cha Vishale (TADA) Innocent Joseph, amesema hayo ni mashindano makubwa chini ya uongozi wao mpya yatafanyika kwa mwaka huu kwenye Bwalo la Magereza mkoani humo na kushirikisha idadi kubwa ya wachezaji.

Amesema yataanza mashindano ngazi ya klabu yatakayoshirikisha wachezaji kutoka mikoa mbalimbali ya Dar es Salaam, Tanga, Mbeya, Kagera, Kilimanjaro, Dodoma na mikoa mingine wanachama wa klabu hiyo.

“Tutaanza na ngazi za klabu tukitegemea kuangalia viwango vya wachezaji wetu. Hapa kutakuwa na wachezaji mmoja mmoja, wawili na kama timu na siku ya mwisho tutafanya yakayoshirikisha timu za taifa,”amesema.

Kwa mujibu wa Joseph, michuano ya pili itakutanisha timu za taifa kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani Kusini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button