PESA inauma sana, hasa unapoona inaenda bure wakati mtoaji alitarajia ingerudi kwa namna alivyoamua kuwekeza kwenye biashara fulani.
Suala hilo limemfanya Naibu Spika, Mussa Azzan Zungu kutoa ya moyoni kwa wachezaji wa Simba SC, ambao wanalipwa pesa nyingi ila uwanjani hamna kitu.
“Wachezaji hawa wana gharama. Mchezaji analipwa fedha nyingi hivyo lazima wajitume.” Amesema Zungu.
Zungu ambaye ni mgeni rasmi kwenye tukio la Unyama Mwingi lililoandaliwa na Simba amesema hayo leo wakati akizungumza kwenye tukio hilo.
Amesema gharama za wachezaji zinalipwa na mwekezaji Mohammed Dewji hivyo wachezaji wanapaswa kufanya kazi ipasavyo.