Wadau wanolewa kusimamia utekelezaji uongezaji virutubishi kwenye vyakula

MOROGORO: OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imesema dhamira ya serikali ni Watanzania kupata vyakula vyenye ubora na virutubishi muhimu kwa ustawi wa afya zao.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe kutoka Tamisemi, Luitfrid Nnally amesema  hayo wakati akiwasilisha salamu kabla ya mgeni rasmi kufungua mafunzo kwa wadau wa wataalamu wa urutubishaji vyakula kutoka taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi nchini.

Mafunzo hayo ya siku nne yanatarajia kufikia tamati Aprili 18, 2025 na yameandaliwa kwa pamoja na Jukwaa la Wadau wa Uongezaji Virutubishi kwenye vyakula nchini ,Wizara ya Viwanda na Biashara ,Wizara ya Afya ,Taasisi ya Food Fortification Initiative,Taasisi ya Chakula na LisheTanzania chini ya uwezeshwaji wa Shirika la UNICEF.

Advertisement

“ Tumekutana hapa katika mafunzo haya kwa ajili ya kujadili mikakati hii , na sina budi kwanza kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ambaye suala la lishe amelipa kipaumbele kikubwa na kauli mbiu yake”Tanzania bila utapiamlo inawezekana “ amesema.

Nnally amesema kuwa kipaumbele hicho ni tangu alipokuwa Makamu wa Rais ambapo aliweza kusainisha mikataba na wakuu wa mikoa waweze  kuhakikisha ya jamii inakuwa na liche bora.

Amepongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kutunga sheria na kupitisha kanuni za uongezaji virutubishi  kwenye vyakula ili viwe na ubora katika kusaidia kupambana na matatizo ya lishe kwa watoto na jamii ya watanzania .

“ Kitendo hiki ni kuunga mkono juhudi za Rais za kuhakikisha kwamba vyakula vina kuwa na ubora wa kusaidia kupambana na matatizo ya lishe kwa watoto na kwa jamii mzima ya watanzania  na wakiwa na afya bora wanaweza kuchangia uchumi wa taifa letu,” amesema  Nnally.

Amesema baada ya mafunzo hayo, jukumu kubwa kwa watendaji na wadau mbalimbali wenye mamlaka ni ufuatiliaji kwa wataalamu waongezaji virutubishi kwenye vyakula ili kuona ubora wa vyakula unakuwa wa viwango vya juu .

Nnally amezishauri Taasisi ya Chakula na Lishe pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kupitia maabara zao kuhakikisha wanapima ubora wa vyakula hivyo ili kuangalia iwapo vina virutubishi wenye usalama kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopitishwa na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Kwa upande wake Ofisa Biashara Mwandamizi ,Wizara ya Viwanda na Biashara  Festo Kapela amesema kama nchi tayari,Aprili 3, mwaka huu zimezunduliwa kanuni ambazo zinaenda kutumika na lengo kubwa ni kuhakikisha unawekwa ulazima katika suala la uongezaji virutubishi kwenye chakula .

Uongezaji wa virutubishi utafanyika kwenye vyakula kama unga wa ngano, unga wa mahindi na chumvi, kwani  kabla sheria na kanuni hizo, wazalishaji wa vyakula kulikuwa na kulaumiana ya kwamba baadhi walikuwa wakiwema virutubishi lakini wengine hawaweki  na kulifanya jambo kuwa ngumu katika utekelezaji wake .

“ Lakini baada ya kanuni kuzunduliwa sasa hivi ni lazima kuongeza virutubishi kwenye chakula na wataalamu wetu kutoka TBS kwa kushirikana na wa Tamisemi wataanza kupita huko,” amesema Kapela.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *