Wafanyabishara wapewa uwezo kutumia masoko nje ya nchi

DAR ES SALAAM: CHEMBA ya Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki wametoa mafunzo kwa wafanyabishara wa Tanzania ili waweze kutumia kikamilifu masoko ya nje ya nchi.

Akizungumza leo wakati akizindua warsha wa mchakato wa kuuza nje ya Nchi na Ukanda wa Afrika Mashairiki Rais wa TCCIA, Vicent Minja amesema wanatambua umuhimu wa kuelewa taratibu za kuuza nje na jinsi zinavyochangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo kupitia mafunzo hayo wananafasi ya kuchambua mifumo ,kubaini changamoto na kutafuta suluhisho zinazoweza kuletea mafanikio makubwa.

Advertisement

“Tunakutana hapa leo kwa lengo la kujifunza ,kubadilisha uzoefu na kufungua milango kuelekea fursa mpya katika biashara ,viwanda na kilimo ,”ameeleza.

Minja amesema katika warsha hiyo wana bahati kubwa ya kuwa na wataalamu ,wafanyabiashara na wadau wa sekta mbalimbali waliohudhuria tukio ambapo ametoa shukrani za pekee kwa Baraza la Biashara Afrika Mashariki kwa ushirikiano wao katika kuandaa warsha huo.

“Kwa niaba ya chemba ya biashara ,viwanda na kilimo Tanzania na wajumbe wa bodi yetu ya wakurugenzi nina imani kubwa katika nguvu ya ushirikiano wetu ,tukijenga mtandao thabiti wa biashara na kushirikiana kwa pamoja tunaweza kufika malengo makubwa zaidi,”amesisitiza.

Ameongeza “Nimejifunza kutoka kwa uzoefu wangu wa mchango wenu kuwa maendeleo yetu yanategemea sana juhudi zenu za pamoja kwahiyo nawasihi nyote mshiriki kikamilifu kwa kuuliza maswali na kubadilishana mawazo yenu.

Kwa upande wake Mfanyabiashara kutoka Kampuni ya ROAF Investiment,ambao ni wauzaji wa asili, Joseph Kimambo amesema anajifunza kuhusu hatua za usafirishaji na hatua zingine na itamsaidia kujua anatakiwa kufanya nini ili aweze kusafirisha bidhaa nje ya nchi kwani watu wengi hawajui vitu vinavyohitajika.

“Hapa leo kuna watu wote wanaohusika na usafirishaji ikiwemo mazao ya kilimo na wengine hivyo nategemea itanisaidia sana,”amesema

1 comments

Comments are closed.