KUANZIA Oktoba 26 hadi Novemba 1 mwaka huu wagombea wa ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa wanatakiwa kujitokeza kuchukua fomu ya kutimiza zoezi hilo.
Hayo amesema Leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mohamed Mchengerwa alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kujitokeze kugombea nafasi mbalimbali za Serikali za Mitaa.
“Oktoba 26 hadi 1 Novemba mwaka huu wagombea wanatakiwa kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea uongozi wa ngazi mbalimbali za serikali,”amesema Mchengerwa.
SOMA: Uchaguzi mitaa kutoa viongozi bora
Pia amesema Novemba 27, 2024 wananchi wajitokeze kupiga kura kuchagua viongozi wanawataka wao ambao watakuwa wawakirishi wao katika kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yao.
Mchengerwa amesema watu milioni 32.9 sawa na asilimia 94.8 wamejitokeza kujiandikisha mwaka huu, ukilinganisha na mwaka 2019 ni sawa na asilimia 86 wamezidi kujitokeza kwa kuitikia wito wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Aidha ameongeza kuwa kuanzia leo 21 Oktoba 2024 wananchi 3anatakiwa kujitokeza kuhakiki majina yao waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku saba.