Wagombea waanza kuchukua fomu za uteuzi

MVOMERO : MGOMBEA kupitia Chama cha Al- liance for Democratic Change (ADC), Jesca Mfumya alifika Ofisi ya Msi- mamizi wa Uchaguzi chini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwenye jimbo hilo kuchukua fomu.

Mfumya alifika katika ofisi hizo eneo la Wami Sokoine, Kata ya Dakawa ambako Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Mary Kayowa alimkabidhi nyaraka ajaze kwa mujibu wa sheria, kanuni na utaratibu. Mgombea mwingine aliyekabidhi- wa fomu za uteuzi kugombea ubunge Jimbo la Mvomero ni wa Chama cha Democratic Party (DP), Fatuma Mohamed.

SOMA: Mgombea urais CUF atangaza vita wezi mali za umma

Pia, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo  alikabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa ubunge kupitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo), Kashikashi Ligowoka. Kayowa aliwahakikishia wagombea hao kuwa INEC ni chombo huru kilichojipanga kuzingatia katiba, sheria na kanuni wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu. 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button