Wajasiriamali kushindanisha bidhaa zao Arusha
WAJASIRIAMALI wa Mkoa wa Arusha wameombwa kujitokeza Septemba 27- 29 mwaka huu ili kuonesha bidhaa wanazozalisha na kuuza kupitia mnada wa kishua ujulikanao kama “Jambo Fair Season 4” utakaofanyika kwenye viwanja vya General Tyre Njiro Jijini Arusha
Akizungumzia tamasha hilo la “Jambo Season 4” au Manda wa Kishua msimu wa nne, Husna Almasy mwenye Taasisi ya Foundation amesema tamasha hilo litafanyika viwanja vya General Tyre Njiro Arusha lengo ni kukuza kazi wanazofanya wajasirimali hao katika kijikwamua kiuchumi na kuinua uchumi wa mmoja mmoja.
SOMA:Wanawake wajasiriamali kuwezeshwa kisasa zaidi
Amewasihi wajasirimali hao kutokeza kwa wingi kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha ili kupata fursa ya kuzitangaza na kuuza kwa wa mbalimbali wakiwemo wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
“Hii ni fursa kwetu ya kuonyesha kazi zetu tunazozalisha ikiwemo kuuza bidhaa zetu na pia itatufungukia njia ya kuuza bidhaa ndani na nje ya nchi,tunamua kuja tamasha hili ili kujikwamua kiuchumi,shime tujitokeze kuonyesha kazi zetu muhimu tunazofanya”