Wakamatwa wizi wa pikipiki sita
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu, Rafael Edward, 30, mkazi wa Lyambogo, Juma Ibrahimu,26, mkazi wa Mwale na Yusufu Wihanji,35, mkazi wa Mwale kwa tuhuma za wizi wa pikipiki sita katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Mbeya.
Pikipiki zilizokamatwa ni MC 139 CNX Sanlg, MC 488 BSJ Sanlg, MC 263 DFM Sanlg, MC 314 ASP Kinglion, pikipiki mbili zisizokuwa na namba za usajili aina ya Kinglion ambazo ni mali za wizi.
SOMA: RC awatunuku vyeti polisi Mbeya
Pikipiki hizo zilikutwa zimefichwa nyumbani kwa mtuhumiwa Yusufu Wihanji, mkazi wa Mwale Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga imeeleza kuwa watuhumiwa wamekiri kuhusika katika matukio ya uporaji na wizi wa pikipiki katika maeneo tofauti wilayani Mbarali.
SOMA: Dk Tulia alipongeza jeshi la polisi Mbeya
Amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.