Wakulima Songwe waanza kunufaika na mgao wa mbolea

Wakulima Wilayani Songwe wameanza kunufuaika na upatikanaji wa mbolea ya ruzuku ambapo Kata za Gua, Kapalala, Ngwala, Saza na Mkwajuni zimenufaika na mgao wa mifuko 10,912 huku mbolea zaidi ikitarajiwa kupokelewa hivi karibuni.

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Simon Simalenga ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo, wakati akimshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha zoezi la upatikanaji wa mbolea hiyo, katika ziara yake leo hii.

“Hakika wananchi wa Wilaya ya Songwe wamejawa na mioyo ya shukrani kupita kiasi kwa Rais wetu mpendwa Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan bila kumsahau Waziri wetu wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kutokana jitihada kubwa zinazoendelea kufanyika kwa Wakulima wa nchi hii na sisi Songwe,” amesema Simalenga.

Advertisement

Amesema licha ya muitikio kwa wananchi wenye uhitaji wa mbolea hiyo kuwa ni mkubwa ila kuna changamoto wa ucheleweshwaji wa mbolea kwa baadhi ya maeneo.
“Nimeshawasilisha kwa Mkuu wetu wa Mkoa, Waziri Kindamba ambaye mara zote amekuwa msaada mkubwa katika kushughulikia masuala ya Songwe kila tunapomshirikisha.” alisema Simalenga.