Walioanza kujipitisha ubunge, udiwani waonywa

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita, Nicolous Kasendamila, amekemea wanachama kuanza kampeni za kunyemelea nafasi za udiwani na ubunge kabla ya wakati, badala yake wasubiri muda utakapofika.

Kasendamila ametoa kalipio hilo, wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM wilayani Chato na kumtaka kila mwanachama kuunga mkono madiwani na wabunge waliopo kutekeleza ilani ya chama.

Amesema tabia ya watu kuanza kampeni mapema inafanya madiwani na wabunge waliopo kushindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha na kukwamisha malengo ya chama na serikali.

“Naelekeza kwamba waacheni madiwani wafanye kazi zao za utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo tumewakabidhi mwaka 2020 hadi 2025 na muda ikifika wa uchaguzi mkuu nafasi zitakuwa wazi, lakini siyo sasa,” amesema.

Amesema CCM ina utaratibu wake wa kuchagua na kupitisha wagombea kwa kuanzia mchakato wa kura za maoni mpaka uchaguzi mkuu, hivyo ni lazima wanachama waheshimu miongozo ya Katiba ya chama na Katiba ya nchi.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button