Wanafunzi Udom watengeneza ‘roketi’

DAR ES SALAAM; CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimefanikiwa kutengeneza roketi ambayo mpaka sasa ina uwezo wa kuruka urefu wa futi 3000 kutoka usawa wa bahari.

Hayo yameelezwa na Dkt. Ramadhan Bakari kutoka Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi chuoni hapo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema wanafunzi wawili kutoka Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi na Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati, wametafiti roketi baada kuona dunia inaenda kwenye sayari za juu na kufanya utafiti kwa kutumia teknolojia hiyo..

Isome pia:https://habarileo.co.tz/wanafunzi-wabuni-roboti-inayotabasamu-darasani/

Dk Bakari amesema wanafunzi hao katika kufanikisha utafiti huo wametumia kanuni mbalimbali za kisayansi, ambapo wamefanikiwa kuitengeneza roketi hiyo kwa kufanya majaribio mbalimbali kwa kutumia vitu vinavyopatikana hapa nchini na kwa bei rahisi.

“Wanafunzi hawa kwanza wametengeneza nishati ya kuendesha chombo hicho na kufanya majaribio mbalimbali, lengo likiwa baada ya hapo waweze kuita satalaiti kwa kutumia roketi hiyo,” amesema.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/watakiwa-kuendeleza-vijana-wabunifu-wa-kisayansi/

Amesema matumaini yao kama chuo, ifike mahali nchi iwe na uwezo wa kuita kitu kwa tutumia roketi yake, lakini pia satalaiti hizo zitengenezwe hapa hapa Tanzania.

Amesema kwa kufanya hivyo nchi itaweza kufanya ufuatiliaji wa usalama wake, lakini pia kufuatilia hali ya hewa ya nchi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button