Wanamichezo sita wapigana vikumbo urais TFF

DAR ES SALAAM; WANAMICHEZO sita wamejitokeza kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Agosti 16, mwaka huu jijini Tanga.


Taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Benjamin Kalume imewataja wanamichezo hao kuwa ni Ally Mayay Tembele, Ally Thabit Mbingo, Mbette Mshindo Msolla, Mustapha Salum Himba, Shija Richard Shija na Rais wa sasa Wallace John Karia.

Pia taarifa imesema wanamichezo 19 wamerudisha fomu kuomba Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia kanda mbalimbali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button