Wananchi 35,000 wanufaika majisafi Babati

MANYARA: Mamlaka ya  Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA) mkoani Manyara imekamilisha mradi wa maji wa Darakuta hadi Minjingu ambao utasaidia kusambaza maji kwa wananchi zaidi ya 35,000 wa kata ya Nkaiti wilayani Babati mkoani humo.

Wakazi hao wameanza kunufaika na huduma ya majisafi na salama baada ya kuanza kusambaza kama sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Maji kati ya Machi 16 hadi Machi 22.

Mkurugenzi Mtendaji wa BAWASA, Mhandisi Idd Msuya amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa kwa gharama  zaidi ya Sh bilioni 16 umejumuisha mtandao wa mabomba wa zaidi ya kilomita 60 kutoka kwenye chanzo hadi kufikisha maji kwa wananchi wa kata za Nkaiti, Mwada, Magugu na Kisangaji waliokuwa wanatumia maji yasiyo safi na salama kwa ukosefu wa maji ya bomba.

“Tumeanza kusambaza maji haya kwa wananchi wa Kata ya Nkaiti kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji kati ya Machi 16 hadi Machi 22,” amesisitiza Msuya.

Meneja Huduma kwa Wateja, Mhandisi Rashid Charahani, amebainisha kwamba mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa zaidi ya Sh bilioni 16 toka ulipoanza Januari mwaka 2025.

Kwa upande wao Saruni Mollel, Diwani wa kata ya Nkaiti, Samwel Lomboi, Mwenyekiti wa kijiji cha Olasiti, na Maria Chambia, mkazi wa kijiji cha Olasiti, wamemshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuukamilisha na kuondoa kero ya upatikanaji wa maji.

Awali wananchi walitembea mwendo mrefu kufuata maji ambapo shughuli za maendeleo zimekuwa zikikwama.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Kama selikali inatambua umuhimu wa uwepo wa maji safi na salama,ni kwanini maji hayo yanakua yanakata kwa muda mrefu katika baadhi ya maeneo na hata maji kuwa machafu. Hivyo basi ningeomba mamlaka zinazohusika na suala hili zingeangalia namna bora ya kufanya ili kuhakikisha kila mtanzania anapata maji safi na salama kwa wakati hasa maeneo ya vijijini ambapo suala hili limekua kero kubwa kwa wananchi wengi.
    natumaini yote hayo yatawekwa kwenye matazamio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button