Wananchi 5,000 kunufaika na mradi wa zahanati mji Handeni

TANGA: ZAIDI ya wananchi 5,000 waliopo katika mitaa mitano ya kata ya Msasa katika Halmashauri ya Mji Handeni wanakwenda kunufaika na huduma bora za afya karibu na eneo lao baada ya kukamilika kwa ujenzi wa zahanati iliyogharimu kiasi cha Sh milioni 102.1.

Akiongea na waandishi wa habari Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Wakili Marium Ukwaju amesema kuwa fedha za ujenzi wa zahanati hiyo zinatokana na fedha za makusanyo ya mapato ya ndani pamoja na mfuko wa jimbo

Amesema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo unatarajiwa kufanyika kwa awamu huku wakianza na ujenzi wa jengo la huduma za nje (OPD ) ili wananchi waweze kupata huduma mapema.

“Kukamilika kwa Zahanati hii ambayo itakuwa na vifaa tiba vya kisasa kutaboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa kuweka mazingira bora ya kupata huduma za afya

Aidha amesema kuwa mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umeweza kufikia asilimia 77 ambapo kazi zilizo baki ni uwekeaji wa miundombinu ya maji ,umeme pamoja na kumalizi kazi ndogondogo (Finishing) ya jengo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button