Wananchi Iringa wafikiwa kampeni NIC Kitaa

IRINGA: Kampeni ya kutoa elimu ya bima mtaani ijulikanayo kama NIC Kitaa imezinduliwa mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo wanayoishi na kufanya shughuli zao.

Kupitia kampeni hiyo, Shirika la Bima la Taifa (NIC) limejipanga kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu umuhimu wa bima za maisha na mali, sambamba na kuwawezesha kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya majanga yanayoweza kutokea bila kutarajiwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi mjini Iringa, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC, Karimu Meshack, alisema dhamira kuu ya kampeni hiyo ni kusogeza huduma za bima karibu na wananchi kwa kuwapa elimu ya moja kwa moja na kujibu maswali yao papo kwa hapo.

Meshack alisema kwamba soko la bima nchini bado ni dogo—likiwa asilimia 2.8 pekee—na moja ya sababu ni wananchi kutofikiwa moja kwa moja na watendaji wa sekta hiyo.

“Usipokuja mtaani unapunguza kasi ya wananchi kujua umuhimu wa bima. Sisi kama shirika kongwe lazima tuoneshe njia. Tumeshuhudia wananchi wanajenga nyumba kwa miaka mingi lakini zinapoteketea wanakosa fidia,” alisema.

Alibainisha kuwa kampeni hiyo ambayo pia imekwishafanyika katika baadhi ya mikoa nchini, safari hii imeelekezwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ukiwemo mkoa wa Iringa na Njombe.

Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James amesema: “Bima ni usalama wa maisha na mali zetu.”

Aliunga mkono kampeni hiyo akibainisha kuwa serikali inaendelea kusukuma agenda ya elimu ya bima kwa wananchi kupitia taasisi zake.

“Bima inatupa usalama wa mali na maisha yetu. Tunajipa uhakika pale mali zinapopotea au tunapopata madhara. Ni muhimu sana taasisi kama NIC kuwafuata wananchi walipo kwenye shughuli zao, masoko na mitaani hasa kwa sababu wengi hawapati muda wa kufuatilia vyombo vya habari,” alisema.

Kheri James alisema wiki nzima ya kampeni mkoani Iringa itatoa fursa ya kutosha kwa wananchi kupata elimu kuhusu namna bima inavyoweza kuwa kinga madhubuti dhidi ya majanga na hasara.

Meneja wa NIC wa mikoa ya Iringa na Njombe, Paul Mkumbo, alifafanua huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo, akisisitiza kuwa wananchi wanaweza kunufaika moja kwa moja ikiwa wataitumia kampeni hii kupata maelezo ya moja kwa moja kutoka kwa wataalamu.

Mkumbo ameeleza kwa kina aina za bima zinazotolewa na NIC, ikiwemo: Bima ya Mali ambayo kazi yake ni kulinda nyumba, biashara, majengo ya taasisi na mali nyingine dhidi ya moto, wizi, mafuriko na majanga mengine.

Nyingine ni bima ya maisha: ambayo hutoa msaada wa kifedha kwa familia endapo mhusika atafariki au kupata ulemavu wa kudumu.

Alitaja bima nyingine kuwa ni zile zinazolinda mkulima, mfanyabiashara au mfanyakazi binafsi dhidi ya ajali au gharama za matibabu, bima ya usafiri na
bima za kibiashara kwa kampuni, viwanda, mashirika na biashara ndogo ndogo zenye uhitaji wa kulinda biashara na vifaa vyake.

Amesema hudumu hizo zinapatikana kwa gharama rafiki, na kampeni ya NIC Kitaa inalenga kuhakikisha wananchi wanaelewa kile wanachokilipia na faida wanazopata.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

  2. How can we Transform “Dreams to diseases and Death” – I have something to say about you (you will get through dreams

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  3. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button