WANANCHI takribani 3,700 katika vijiji vya Mbobole na Sakale wilayani Muheza mkoani Tanga watanufaika na mradi wa maji safi wenye thamani ya zaidi ya Sh milioi 877.
Akizungumzia na Wananchi wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi katika mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kila Mwananchi mjini na vijijini anapata huduma ya maji safi na salama.
“Niwaombe Wananchi wanaishi kwenye vyanzo vya maji kutokufanya uharibifu kwenye maeneo ya vyanzo na kulinda na kutunza miundombinu hii idumu kwa muda mrefu.”amesema RC Kindamba.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Mjini na Vijijini Mkoa wa Tanga, Mhandisi Upendo Lugongo amesema kuwa mradi utakapokamilika utazalisha lita 150,000 huku mahitaji ya Wananchi wa vijiji hivyo ikiwa ni lita 90,000 pekee.
“Mradi huu kwa sasa umefikia asilimia 72 na utakapokamilika utasaidia kupunguza adha ya uhaba wa maji na kupunguza kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.”amesema Mhandisi Lugongo
Comments are closed.