Wananchi kupimwa bure magonjwa ya moyo

DAR ES SALAAM; HOSPITALI  ya  DSB Polyclinic kwa kushirikiana na Taasis ya Heart of Foundation of  Tanzania,  zimeandaa kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma ya  upimaji na matibabu bila malipo ya magonjwa ya moyo na magonjwa mengine kwa watu wazima na watoto Dar es Salaam.

Kambi hiyo inaanza kesho Novemba 4, 2023 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 11 jioni  katika hospitali ya DSB Upanga na watakaokutwa na matatizo watapatiwa dawa.

Daktari kiongozi wa DSB, Issa Mbashu amesema  huduma zitakazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na  upimaji wa shinikizo la damu, upimaji wa sukari kwenye damu, upimaji wa uwiano wa urefu na uzito, upimaji wa oksijeni mwilini na kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo.

Amesema vipimo vingine ni kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, kipimo cha  msongo wa mawazo (stress), ushauri wa daktari bingwa wa moyo, elimu na ushauri wa lishe bora na upatikanaji wa dawa kwa wale watakaokutwa na matatizo kupatiwa dawa.

Amesema kambi hiyo inafuatia  maadhimisho  ya  siku ya kiharusi duniani yaliyofanyika  Oktoba 29, na kuwataka wananchi kufika kwa wingi ili kupata matibabu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
LiliaHood
LiliaHood
29 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 29 days ago by LiliaHood
Julia
Julia
29 days ago

Cash generating easy and fast method to work in part time and earn extra $15,000 or even more than this online. By working in my spare time i made $17,000 in my previous month and i am very happy now because of this job.
.
.
Detail Here——————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x