Wananchi Misusugu wasogezewa huduma mama na mtoto

WANANCHI wa kata ya Misusugu wilayani Kibaha mkoani Pwani wanatarajiwa kuondokana na tatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya ya mama na mtoto baada ya ujenzi wa jengo la huduma hiyo kuanza.

Hayo yalibainishwa na ofisa maendeleo ya jamii wa kata hiyo, Kezia Olambo, wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya ukamikisha wa jengo hilo, katika zoezi la kuhadhimisha wiki ya kutoa shukurani Kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Alisema wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za mama kujifungua katika eneo la Malandizi na hopstali ya rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi jambo ambalo limekuwa likichangia kuongea Vifo vya mama na mtoto.

“TRA tunawashukuru Kwa kutupatia msaada wa vifaa hivi vya ujenzi maana ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati hii itaokoa maisha ya wanawake wanahitaji huduma ya kujifungua maana wengi wamekuwa wakitoka hapa kwenda kufuata huduma mlandizi au hosptali ya rufaa ya mkoa wa Pwani”alisema

Awali akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Meneja wa malaka ya mapato Tanzania, Mkoa wa Pwani, Masawa Masatu, alisema wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo , Kokoto, Nondo tani moja, matifali 1,500 pamoja na mifuko ya saruji.

“Tupo katika wiki ya kutoa shukurani Kwa walipa kodi ambayo imeanza leo ,Disemba Mosi hadi Disemba 07,2023 ambapo tumekabidhi msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni sita…wanakuja kupata huduma hapa ni walipa kodi wetu na ni sehemu ya shkrani zetu”alisema

Aidha alisema ni wajibu wa kila mtanza kujijengea destu ya kulipa Kodi Kwa hiyari pasipo kushurutishwa na kwamba Kodi hiyo ndio zinazosaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa ikiondoa adha mbalimbali Kwa jamii na kwamba TRA imetenga zaidi ya Sh milioni 9 kutoa misaada kwa wananchi.

Naye Afisa mtend wa kata hiyo, Elizabeth Mwakalikwa, alisema ujenzi wa jengo Hilo utagaharimu zaidi ya shilingi milioni 60, na kwamba bado jitihada za makusudi zinahitajika ili kumalizia ujenzi huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kukamilisha mradi huo.

“TRA wametupatia msaada na tunamshukuru na kupitia msaada huu tutaendelea kuhamasisha wananchi kulipa Kodi Kwa ajili ya maendeleo yetu wenye…ujenzi huu bado haijakamilika tunaomba wadau wengine wajitokeze kutoa misaada ambayo itusaidia”alisema

Swaiba Kaisi mkazi wa kata ya misugusu, alisema kukamilika Kwa ujenzi wa jengo Hilo litakuwa mkombo Kwa wanawake kuondokana na adhamba ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma umbali mrefu ambapo utapunguza vifo vya wanawake wajawazito.

Katika hatua nyingine mamlaka hiyo imetoa msaada wa vyakuka na vinywaji katika kituo Cha watoto yatima cha Fadhillah Ophanage Center ambayo ni, sabuni, unga, Mchele, mafuta, sukari na mahitaji mengi ya msingi.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button