Wananchi walalamikia viingilio Sabasaba

DAR ES SALAAM: MAELFU ya Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam na mikoa jirani wamejitokeza katika kilele Cha Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2024) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali baadhi ya wananchi walioshiriki pamoja na kupongeza wamesema changamoto kubwa ni viingilio vikubwa hivyo wameomba Serikali kuona umuhimu wakuvipunguza ili washiriki na familia zao.

“Kiingilio kilikuwa mkubwa Sh 3000 na mtoto Sh 1000 ila leo mkubwa ni Sh 4000 na mtoto ileile buku,” amesema mmoja wa watembeleaji.

Advertisement

SOMA: Samia, Nyusi watembelea mabanda Sabasaba

Wasimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia kwa Meneja wa Kanda ya Mashariki Zakaria Muyengi wamewaomba Watoa huduma za Bima Nchini kutumia Maonesho hayo kupata Elimu zaidi ili kuboresha huduma zao huku

Magreth Mngumi Msajili wa Malalamiko kutoka ofisi ya Msuluhishi wa migogoro ya bima (TIO) akiwaomba Watumiaji wa huduma kupeleka malalamiko yao ili yapatiwe majibu haraka.

Nao Watoa huduma za Bima Kutoka BUMACO Hilda Swai na Happy Lema wamewaomba Watanzania kuendelea kutumia huduma mbalimbali za Bima zinazotolewa na Kampuni ikiwemo Bima ya Maisha na vyombo vya moto Ili waweze kufikia ndoto zao ikiwa ni pamoja na kukuza Uchumi wao.

Maonesho hao ya Biashara yalifunguliwa Juni 28 mwaka huu, yakafunguliwa rasmi Julai 3 na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 13 mwaka huu.