‘Wananchi wamechangia mabadiliko viongozi Mtwara’

MTWARA; SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini, imesema panguapangua ya baadhi ya viongozi mkoani Mtwara imesababishwa na wananchi wenyewe.

Katibu Msaidizi wa Sekretarieti hiyo Kanda ya Kusini, Philoteus Manula, amesema hayo wakati wa hafla ya kuapisha waku wa Wilaya za Mtwara na Nanyumbu mkoani Mtwara.

Amesema wananchi wanapeleka taarifa kwa sekretarieti hiyo kuhusu mienendo na tabia za viongozi wa umma juu ya utekelezaji wa majukumu, ambayo wamepewa na serikali kwa mujibu wa sheria.

Advertisement

“Panguapangua ya Mtwara imesababishwa na wananchi wenyewe, wanatuletea taarifa tunafuatilia na kuangalia hali halisi kitu kinachofanyika na hao viongozi,” amesema.

Manula amesema kuwa sekretarieti hiyo imekuwa ikifuatilia tabia ya viongozi na wakiona kwamba haendani na yale ambayo wameelekezwa kwa mujibu sheria na maelekezo ya Rais ambayo anayatoa kwa viongozi hao wanachukua hatua ya kupeleka taarifa kwenye mamlaka.

Panguapangua ya baadhi ya viongozi akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, ilitokea baada ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan Kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Mtwara.

3 comments

Comments are closed.