Wananchi waondolewa ajali ya lori la mafuta kongwa

MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remedius Mwema Emmanuel amesema mamlaka wilayani humo zimefanikiwa kuondoa umati wa wananchi uliokuwa umevamia lori la mafuta lililopinduka ili kujipatia mafuta.

Mapema leo, Habarileo ilichapisha habari kuwa lori la mafuta limepata ajali Gairo na kwamba askari walishindwa kuzuia umati wa watu kufika katika eneo hilo.

Idadi kubwa ya wananchi, wengi wakiwa wamebeba ndoo na vidumu walionekana kuzingira liri la mafuta lililopinduka huko Kongwa eneo karibu na Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

“Nimefika eneo la tukio, awali ilisemekana ni Gairo lakini ni Kongwa.

Tumefanikiwa kuwaondoa wananchi katika lori hilo na taratibu zingine za kiusalama zinaendelea,” amesema DC Mwema.

Habari Zifananazo

Back to top button