Wananchi watakiwa kutoa taarifa utapeli mitandaoni
ARUSHA: WANANCHI wanaotapeliwa kwa njia ya mitandao ya simu wametakiwa kutoa taarifa polisi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili wahusika wachukuliwe hatua kukomesha suala hilo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni mpya ya ‘Sitapeliki’.
SOMA ZAIDI: Rama Ngozi: Aelezea njia kujikinga na wizi mitandaoni
Amesema endapo taarifa za utapeli zikitolewa kwa Jeshi la Polisi mamlaka husika zinaingia kazini kusaka matapeli wanaoibia wananchi kupitia simu za kiganjani.
Amesema kadri teknolojia inavyokuwa ndio matapeli wanavyobuni utapeli kwanjia ya mtandao lakini matapeli hawana nguvu kubwa bali wanatumia maendeleo ya teknolojia kutapeli watu lakini na nyie wanna msikubali kutapeliwa namba zinazotumika ni 100 pekee katika kuwasiliana na wahudumu.
Aidha, Waziri Silaa ameahidi kushirikiana na kampuni za mitandao ya simu pamoja na TCRA ilu kuboresha kitengo cha huduma kwa wateja wahudumiwe kwa wakati badala ya kutumia muda mrefu huku watoa huduma wakisema simu yako inaendelea kurekodiwa tafadhali endele kusubiri



