Korea Kusini wafadhili ujenzi mtambo bayogesi Monduli

TAASISI ya Wanasayansi Wahandisi Wasio na Mipaka (SEWB) ya Korea Kusini imefadhili ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi asilia ya kupikia ya bayogesi katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Monduli mkoani Arusha kwa gharama ya Sh milioni 124.

Uzinduzi wa mtambo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Msaidizi, Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Erick Mgaya kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo. Profesa Nombo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Dk Mgaya amesema  mradi huo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kufanikisha matumizi ya nishati safi na endelevu ya kupikia nchini.

Amesema ufadhili wa mradi huo kutoka SEWB ni mfano wa ushirikiano kati ya mataifa na taasisi katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii. “Teknolojia hii ya bayogesi inapunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa kuwa mtambo utatumia taka za kaboni na mabaki ya chakula kuzalisha nishati safi ya kupikia pamoja na matumizi mengine chuoni hapa,” alisema Profesa Nombo.

Ameongeza kuwa teknolojia hiyo inasaidia kulinda misitu na mazingira, kupunguza gharama za nishati kwa taasisi na kuwapa wanafunzi mafunzo ya vitendo katika teknolojia za nishati jadidifu. Mradi huo unaifanya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwa sehemu ya suluhisho la kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuchochea maendeleo endelevu.

Mkuu wa Chuo cha Veta Monduli, Theophan Pantaley amesema mradi huo umefadhiliwa na SEWB kwa gharama ya Dola za Marekani 49,700 sawa na Sh milioni 124.3. Amesema  mtambo huo una uwezo wa kuzalisha meta za ujazo 100 za bayogesi kwa siku, kiasi kinachoweza kuhudumia wanafunzi 600.

Mkurugenzi wa SEWB, Profesa Minsoo Maeng amesema shughuli za taasisi hiyo zinaendana na sera ya nishati safi ya Tanzania inayolenga kupanua upatikanaji wa nishati salama, nafuu na endelevu ya kupikia. Amesema Serikali ya Jamhuri ya Korea na Serikali ya Tanzania zimeendelea kudumisha ushirikiano katika sekta za elimu, sayansi, teknolojia na maendeleo endelevu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eniart Mahundi amesema mradi huo ni wa pili kufanyika ndani ya Veta kwa ufadhili wa SEWB. Amesema mradi wa kwanza ulitekelezwa katika Chuo cha Ufundi Stadi Arusha (Oljoro) kwa gharama ya Sh milioni 156.8. Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini, Monica Mbele aliutaka uongozi wa chuo na wanafunzi kuutunza mradi huo ambao ni rasilimali ya umma ili udumu kwa muda mrefu.

Ujenzi wa mtambo huo ulifanywa na Kampuni ya Kitanzania ya ENVSOL Technology Agosti mwaka jana na umekamilika Januari mwaka huu. SOMA: REA yatoa majiko ya gesi 310 kwa maafisa magereza Geita

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Start now generating extra home based cash by doing very easy and simple job from home. Last month i have earned $19753 from this job in my part time. This job is just awesome and its earning are greater than 9 to 5 office job. Join this right now by follow instructions here…

    >>>>>>>>>> http://www.giftpay7.vip

  2. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  3. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button