Wang’aka kina ronaldo kupewa laini ya Simu

IRAN,Tehran: Iran inataka kumpa laini ya simu (SIM Card), Cristiano Ronaldo na wachezaji wengine wa soka wa kigeni ili kuwawezesha kutumia mtandao bila vikwazo watakapokuwa Tehran, huduma ambayo raia wa kawaida wa Iran hawawezi kufanya jambo linaloelezwa kuwakasirisha baadhi ya Wairan.
Reza Darvish, Rais wa Persepolis FC, klabu ya kandanda ambayo itamenyana na Al Nassr ya Ronaldo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya AFC juma lijalo, mjini Tehran.
Kiongozi huyo, kupitia kituo cha luninga cha taifa siku ya jana amenukuliwa akisema “baadhi ya watu wanaotaka kuharibu sifa yetu wanawaambia wanasoka wasije Iran kwa sababu hawataweza kufikia mtandao ambao haujachujwa”.
“Nimezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Irancell (mtoa huduma mkuu wa simu), na nikamwambia tunataka kuwapa wachezaji na wafanyakazi laini za Irancell zenye intaneti isiyo na kikomo ili wazitumie kuanzia wanapoingia Iran hadi wakati wa kuondoka,” amesema.
Mtandao nchini Iran umewekewa vikwazo vikali, makumi kwa maelfu ya tovuti na majukwaa yote makuu ya kimataifa ya mawasiliano na mitandao ya kijamii yamezuiwa.
Vizuizi viliongezwa kwa kiasi kubwa baada ya katikati ya Septemba 2022 ilipoibuka ghadhabu ya watu kufuatia kifo cha Mahsa Amini aliyefia mikononi mwa polisi na kusababisha maandamano nchini kote ambayo yalidumu kwa miezi kadhaa.
Aidha, mamlaka nchini humo zilidai kuwa majukwaa ya kigeni, yalikuwa yanatumiwa kuhatarisha usalama wa taifa, kwa kilichoelezwa kuunga mkono ‘machafuko’ ndani ya mipaka ya Iran.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button