Wanne wafa, lori likigongana na coaster

MUHEZA, Tanga – Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori la mizigo kugonga basi dogo la abiria “Coaster” katika eneo la Tanganyika, wilayani Muheza mkoani Tanga.

Lori hilo lenye namba za usajili T 925 CAU liliiparamia Coaster aina ya Nissan Civilian T 228 DPD iliyokuwa imeharibika barabarani wakati likitoka Muheza kuelekea Tanga Mjini.

Kamanda wa Polisi ACP Maket Msangi amesema ajali hiyo imetokea June 15, 2024 majira ya Saa 3 usiku ambapo Jeshi linaendelea kumsaka dereva wa lori la mizigo aliyetambulika kwa jina la Alvis Livingston pamoja na dereva wa Coaster ambaye jina lake halijafahamika.

SOMA: 2023: Watu wanne walikufa kwa ajili kila siku 

Kamanda amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Anwar Juma (30) kondakta, Shabi Omari (45) abiria, Hassan Abdallah (32) na mwanamme mmoja ambaye bado jina lake halijatambulika ambae anakadiriwa kuwa na umriwa  kati ya miaka 25 na 30.

Majeruhi katika tukio hilo ni wanne ambao ni Juma Adam, Hussein Kombo, Mundhir Mwait na Sikujua Hamid ambao hali zao ni nzuri na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali teule Muheza.

Habari Zifananazo

Back to top button