Wanolewa kukabili uhalifu wa mazingira

DAR ES SALAAM: Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Italia ( Sant’Anna School of Advanced Studies -Scuola) wanatoa mafunzo ya siku tatu kwa maofisa wa mahakama na waendesha mashtaka wa Tanzania ili kukabiliana na uhalifu wa mazingira na kuimarisha ushirikiano.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Machi 30, 2026 na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha masuala ya familia na mirathi -Temeke jijini Dar es Salaam, Mwanabaraka Mnyukwa kwa niaba ya Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Dk Paul Kihwelo.

Washiriki wa mafunzo hayo ni majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, mahakimu wakazi waandamizi na waendesha mashtaka.

Lengo lingine la mafunzo kuwajengea uwezo washiriki kuelewa na kutumia mifumo ya kisheria inayosimamia ulinzi wa mazingira, ikiwemo mikataba ya kimataifa na sheria za Tanzania zinazohusu rasilimali kama misitu, wanyamapori na mazingira kwa ujumla.

Katika hotuba ya Dk Kihwelo amesema kuwa uhalifu wa mazingira umeendelea kuwa tishio kubwa duniani, ukihatarisha bioanuai, maendeleo endelevu pamoja na afya na usalama wa binadamu.

Ameongeza kuwa licha ya jitihada zilizopunguza ujangili wa wanyamapori hasa wa tembo, vitendo vya ukataji miti holela na biashara ya mkaa vinaendelea kuongezeka, hasa katika maeneo ya mijini kama Dar es Salaam.

“Ni muhimu kwa maafisa wa Mahakama na Waendesha Mashtaka kuwa na uelewa mpana wa sheria na mbinu za kushughulikia mashauri haya, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa kuwa uhalifu huu sasa unavuka mipaka ya nchi,” amesema Dk Kihwelo.

Pia Dk Kihwelo amewahimiza washiriki kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ili kunufaika na ujuzi utakaowawezesha kushughulikia mashauri ya uhalifu wa mazingira kwa ufanisi zaidi.

Aidha, ametoa shukrani kwa Scuola na Serikali ya Italia kwa ushirikiano na dhamira yao madhubuti katika kuimarisha ujuzi na uelewa wa Maafisa wa Mahakama na waendesha mashtaka katika kukabiliana na makosa mbalimbali ya kuvuka mipaka.

Kwa upande wake, Martina Crisanti, Ofisa Mradi anayewakilisha Chuo cha Sant’Anna, amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya mpango unaoitwa “Utawala wa Sheria na Ushirikiano wa Kimahakama barani Afrika,” unaofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Italia, wenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimahakama na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma miongoni mwa maafisa wa mahakama.

Naye Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Mhe. Amos Rweikiza amesema kuwa anatarajia kuwa mafunzo haya yatawapa mwanga, kubaini changamoto zinazohusu uhalifu wa mazingira na namna ya kushughulikia mashauri yake.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni majaji kutoka Tanzania pamoja na wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Italia.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya IJA na Scuola katika kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama na Waendesha Mashtaka ambapo Septemba 2025, ziliendesha mafunzo yaliyohusu kukabiliana na makosa yanayovuka mipaka yakiwemo ya makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, dawa za kulevya, utakatishaji wa fedha, ugaidi, biashara haramu ya silaha, ujangili, na uhalifu mitandaoni.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,

    This is what I do….. http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button