Washauriwa kutumia taasisi rasmi huduma za fedha
WANANCHI Halmashauri ya Mlimba iliyopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro wametakiwa kuhakikisha wanatumia taasisi za huduma ndogo za fedha ambazo zimeidhinishwa kisheria kufanya shughuli hizo nchini kwa mujibu wa sheria.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba, Neuster Ngelela amesema hayo leo kwenye akiwa kwenye program ya elimu ya fedha inayoendeshwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha nchini.
SOMA: Mbunge aipa tano serikali ujenzi wa barabara
Ngelela amesema hatua ya kuzitumia taasisi za huduma ndogo za fedha kutawezesha kupunguza migogoro kati ya wananchi na watoa huduma ndogo za fedha kunakotokana na kasi ya maendeleo ambapo kila mtu amekuwa na uhitaji mkubwa wa fedha.
TAHARUKI !!! WANANCHI WALIVYOBOMOLEWA NYUMBA ZAO MLIMBA
Wananchi 89 wa kijiji cha ihenga kata ya mofu halmashauri ya mlimba mkoani morogoro wakiwemo watoto, wanalala nje baada ya nyumba zao kubomolewa na nyingine kuchomwa moto chini ya dalali wa mahakama..https://t.co/Mqt4CIswtz— HabariLeo (@HabariLeo) August 22, 2023
“ Ni vyema wananchi mkajielekeza kupata huduma hizo katika taasisi za fedha zilizo rasmi na zilizosajiliwa na kupewa leseni ya kuendesha shughuli hizo ili kupunguza migogoro” amesema Ngelela.
Amesema katika maisha ya sasa kila jambo ni fedha, hivyo ni vyema kila anayehitaji kupata huduma ya fedha iwe ni kukopa au kuwekeza ni vyema akaenda kupata huduma hizo katika taasisi zilizosajiwa kutoa huduma hizo.
SOMA: Malima ahimiza kilimo cha mazao ya kimkakati Mlimba
“ Lengo ni kuwa hata ikitokea mgogoro iwe rahisi mwananchi kupata haki yake, kwani serikali haipendi wananchi wake waingie kwenye migogoro itakayowapotezea muda wa uzalishaji mali’’ amesema Ngelela.
Diwani wa Viti Maalum, Reniter Limba amewashukuru waratibu wa programu kwa elimu wanayoitoa kuwa itasaidia kupunguza wimbi la utapeli unaofanywa na baadhi ya watoa huduma za fedha ambao sio waaminifu.
Program ya kutoa elimu ya fedha kwa umma imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha nchini ikiwa ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha wa mwaka 2020/21-2029/30.