Wasimamizi wa uchaguzi Ilemela wapewa mafunzo

MWANZA: HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imetoa mafunzo kwa wasimamizi na wasaidizi wa vituo 2870 kutoka manispaa hiyo.

Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kuisha kesho. Wasimamizi hao watasimamia Uchaguzi Mkuu katika vituo 944 ambavyo vinapatikana katika kata 19 za halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Ilemela, Herbert Bilia amewaomba wasimamizi kuzingatia maadili ya kazi na kuwa waaminifu wakati wote.

“Someni kwa umakini Katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizeni ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine pengine yatakuwa na changamoto za kufahamu ili kuwarahisishia katika utekelezaji wenu wa kazi za uchaguzi,” amesema.

Amewaomba wasimamizi kujiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kwa kushirikiana vyema na mawakala wa vyama vya siasa watakaokuwepo vituoni kwa mujibu wa sheria.

Amewataka kusoma kwa umakini Katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

“Tumewapa nyaraka mbalimbali ili mzitumie kama rejea kwa kipindi chote cha utekelezaji wa jukumu hili. Jitahidini na mjiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kwa kushirikiana vyema na mawakala wa vyama vya siasa watakaokuwepo vituoni kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Bilia amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kikatiba na kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa hasa katika ngazi ya kituo ambapo mchakato wa kupiga kura na kuhesabu kura huendeshwa na hatimaye, matokeo ya uchaguzi kwa kiti cha Rais, ubunge na udiwani ndio yanapoanzia.

Naye msimamizi kutoka kata ya Kirumba, Fatma Abdallah ameahidi atazingatia mafunzo waliopewa na kusimamia uchaguzi kwa Uhuru na haki. Amewaomba wapiga kura wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button