Wasioendeleza vitalu uchimbaji madini hatarini kupokwa maeneo

MOROGORO: MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amewaagiza wawekezaji waliochukua vitalu vya uchimbaji madini kwa muda mrefu mkoani humo bila kuviendeleza kwamba serikali haitasita kuyachukua maeneo hayo na kuwapa wengine wayaendeleze.

RC Malima ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa wawekezaji wa mkoa huo uliofanyika mjini Morogoro ambao umewashirikisha wataalam mbalimbali wa mkoa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), wawekezaji na wadau wa sekta mbalimbali.

Mkuu wa mkoa amesema wapo wawekezaji wa madini wamepatiwa maeneo ya uchimbaji lakini muda mrefu hawajayaendeleza hivyo mkakati wa serikali ya mkoa kwa sasa ni kuwanyang’anya na kuwapatia wawekezaji wengine.

SOMA ZAIDI: Wanawake wapatiwa leseni 355 uchimbaji madini Geita

Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji, Dk Binilith Mahenge amesema moja ya vivutio vya uwekezaji ni pamoja na kuwepo kwa ardhi iliyopimwa.

Hivyo amewaomba wakurugenzi wa halmashauri kupima maeneo kwa ajili ya uwekezaji huku akiwataka wawekezaji wazawa kujisajili na kusajili miradi yao ya uwekezaji ili wanufaika na fursa zinazotolewa na serikali sawa na wawekezaji wa kutoka nje ya nchi.

Mmoja wa wawekezaji katika sekta ya kilimo, Sifuni Mchome ameeleza namna kampuni yao walivyojipanga kuwekeza mkoani Morogoro katika sekta hiyo hususani ya kiwanda cha kuzalisha viuatilifu wa kilimo na kinu cha kuchakata pamba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button