‘Muwe mabalozi wa amani’

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira amewataka wanachama wa chama hicho kuwa mabalozi wa amani ndani na nje ya chama kwa kuepuka mivutano isiyo ya lazima.

Wasira ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za CCM Mkoa wa Geita iliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita. Amesema wanachama wa CCM wanapaswa kuwa vinara wa kulinda na kudumisha amani kwa kujenga ustahimilivu kabla, wakati na baada ya chaguzi, ndani na nje ya chama.

Aidha, amewaonya wanachama wanaokosa nafasi za uteuzi kuepuka kuwa chanzo cha vurugu au migogoro, akisisitiza kuwa kuvurugika kwa amani kunaweza kuhatarisha usalama wa watu na ustawi wa taifa. SOMA: Ni Wasira Makamu Mwenyekiti CCM Bara

Wasira pia amezitaka ofisi za CCM kote nchini kutumika kama vituo vya elimu kwa wanachama kuhusu misingi na Katiba ya chama, pamoja na kuwa maeneo ya kuimarisha mshikamano badala ya kuleta mgawanyiko. “Ni muhimu kuwaleta watu pamoja na kuwaelimisha ili waelewe chama chao kinataka nini, kwani katika chama hiki elimu haina mwisho,” amesema.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wanachama kuifahamu Katiba ya CCM, malengo, pamoja na mwelekeo wa chama, ili waweze kuchagua viongozi wanaofaa na wenye uwezo wa kukifikisha chama kwenye malengo yake. Kwa mujibu wa Wasira, uchaguzi haupaswi kuwa chanzo cha migawanyiko, bali ni njia ya kupata viongozi na wawakilishi wa wananchi.

Amesisitiza kuwa CCM haitavumilia kuona uchaguzi unaleta mpasuko ndani ya chama au taifa. “Dhamira kuu ya chama chetu ni kushika dola, lakini zaidi ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo,” amesema.

Pia amewataka wanachama kuwa na uvumilivu wakati wa uchaguzi, akibainisha kuwa kushindwa ni sehemu ya mchakato wa kidemokrasia. “Uchaguzi una gharama zake, mojawapo ikiwa ni kukubali matokeo. Kushindwa na kukasirika ni hasara inayopaswa kuepukwa,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa matukio ya uchaguzi yaliyotokea Oktoba 29, 2025 yanapaswa kuangaliwa kama sehemu ya historia iliyopita, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea na maisha na kujenga taifa.Katika hatua nyingine, Wasira amepongeza juhudi za ujenzi wa ofisi za kisasa za CCM Mkoa wa Geita kupitia michango ya wanachama na wadau, akisema hatua hiyo inaonesha kuwa chama kinajengwa kwa nguvu za wanachama wake.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. S­­t­­a­­r­­t m­­a­­k­­i­­n­­g c­­a­­s­­h r­­i­­g­­h­­t n­­­­ow­­… G­­e­­t m­­o­­r­­e t­­i­­m­­e w­­i­­t­­h y­­o­­­­u­­r f­­a­­m­­i­­l­­y b­­y d­­o­­i­­n­­g j­­o­­b­­s t­­h­­a­­t o­­n­­l­­y r­­e­­q­­u­­i­­r­­e ­­f­­o­­r y­­o­­u­­ t­­o ­­h­­a­­v­­e a c­­o­­m­­p­­u­­t­­e­­r a­­n­­d a­­n i­­n­­t­­e­­r­­n­­e­­t a­­c­­c­­e­­ss ­­­­a­­n­­­­d ­­y­­o­­u ­­c­­a­­n h­­a­­v­­e t­­h­­­­a­­t ­­a­­t y­­o­­u­­r h­­o­­m­­e. S­­t­­a­­rvt b­­r­­i­­n­­g­­i­­n­­g ­­u­­p t­­o $­­18­­0­­1­­2 ­­a m­­o­­n­­t­­h. I’v­­e s­­t­­a­­r­­t­­e­­d t­­h­­i­­s j­­o­­b a­­n­­d I’v­­e n­­e­­v­­e­­r b­­e­­e­­n h­­a­­p­­p­­i­­e­­r a­­n­­d­­ n­­o­­w I a­­m s­­h­­a­­r­­i­­n­­g i­­t w­­i­­t­­h y­­o­­u, s­­o­­ yo­­u c­­a­­n t­­r­­y i­­t t­­o­­o. Y­­o­­u c­­a­­n c­­h­­e­­ck i­­t ou­­t h­­er­­e…

    HERE→→→→→ https://PayAtHome1.Com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button