Watakiwa kuongeza ubunifu maeneo ya kazi

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) , Daniel Chongolo amewaagiza maofisa mawasiliano serikalini kuongeza ubunifu kuhakikisha wanayaelewa maeneo wanayoyafanyia kazi pamoja na kuitumia ipasavyo mitandao ya kijamii ili kuhabarisha umma juu ya wapi serikali ilipotoka,ilipo na inapoelekea.

Chongolo alitoa rai hiyo wilayani Karatu mkoani Arusha aliposhiriki kikao kazi cha mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa mkoa wa huo.

Amesema viongozi wengi wamekuwa wepesi kukimbilia vyombo vya habari kuelezea kero za maeneo wanayoyaongoza, lakini serikali inapotatua kero hizo wamekuwa wazito kutumia vyombo vya habari au vitengo vya habari na mawasiliano serikalini kuelezea namna serikali ilivyotatua kero hiyo ili watanzania waelewe.

Amesema pamoja na mambo mengine serikali inayoongozwa na CCM imekuwa ikipelekeka fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa wananchi lakini changamoto imekuwa ni kwa baadhi ya maeneo kutovitumia ipasavyo vitengo vya habari na mawasiliano serikalini kwaajili ya kutangaza mafanikio hayo.

Habari Zifananazo

Back to top button