Watakiwa kutenga muda kuzungumza na watoto

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amewataka wazazi na walezi kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao mara kwa mara, badala ya kuwawekea katuni kwenye runinga huku watoto wakiendelea kuharibika kimaadili.

Buswelu ametoa wito huo katika maadhimisho ya siku ya familia duniani yaliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya shule ya msingi Ifukutwa, Halmashauri ya Tanganyika, mkoani Katavi.

Amesema yapo mambo yanafanywa na jamii yasiyompendeza Mungu, akitaja baadhi kuwa ni mapenzi ya jinsia moja pamoja na vitendo vya ukatili na ukichunguza vinatokana na kukosekana kwa maadili, hivyo ipo haja ya wazazi na walezi kuwatengenezea misingi mizuri watoto wao kabla hawajaharibika.

“Ili haya yatuepuke lazima turejee kwenye kuwekeza kwenye utu, ubinaadamu, upendo na umoja, tuyajenge maadili ya Taifa letu kuanzia ngazi ya familia,” amesema.

Naye mzee Hassan Mapengo mkazi wa wilaya hiyo, amesema zamani wazazi walikuwa na utamaduni wa kukutana na watoto wao ndiyo maana hapakuwa na matendo ya unyang’anyi, kuporomoka kwa maadili tofauti na sasa ambapo wazazi hawana muda wa kuzungumza na watoto zaidi wanarudi usiku kutoka kwenye shughuli zao.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x