Watatu mbaroni, mauaji ya mfanyakazi wa ndani

MOROGORO: Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limewakamata watuhumiwa watatu wa mauaji ya Monica Paul (22), mfanyakazi wa kazi za ndani, mkazi wa Lukuyu bigwa mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP, Alex Mkama amesema watuhumiwa hao walifanya mauaji hayo Aprili 14, 2024 maeneo ya Lukuyu Kata ya Bigwa Wilaya na Mkoa Morogoro.

Aidha,SACP Mkama amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mbaraka Omary (25) fundi ujenzi, mkazi wa Tubuyu.

Pia, amemtaja mtuhumiwa mwingine ni Mussa Mrisho (23) fundi ujenzi, mkazi wa Bigwa ambaye alishirikiana na Mbaraka Omary kutekeleza mauaji hayo pamoja na Rehema Omary (30) mkulima, mkazi wa Mwembesongo, aliyekutwa na simu ndogo ya marehemu aina ya Tecno.

Katika muendelezo wa operesheni hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mororogoro limewakamata watu wawili ambao waliiba pikipiki katika Wilaya ya Morogoro na Kilosa,

SACP Mkama amewataja watuhumiwa hao ni Medson Msowela (27) Mkulima na mkazi wa Mvumi Wilaya Kilosa aliyekamatwa na pikipiki yenye namba za usajili MC 710 EFK aina ya Houjue.

Mtuhumiwa mwingine ni Ally Waziri (30) Mfanyabiashara, mkazi wa Dumila akiwa na pikipiki yenye namba za usajili MC442 EEL aina ya Houjue.

Habari Zifananazo

Back to top button