Watoto 30 wafanyiwa upasuaji wa moyo

DAR-ES-SALAAM : JUMLA ya watoto 30 wamefanyiwa upasuaji wa moyo kati ya watoto 50 waliofanyiwa uchunguzi  katika kambi ya siku 10 iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI,Dk Tatizo Waane amesema kambi hiyo imefanywa na madaktari kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid kwa kushirikiana na wataalamu wa JKCI.

“Huu ugeni umekuwa ukija mara kwa mara

Matibabu hayo ni muhimu yanaokoa gharama timu hii ya wataalamu kwa kushirikiana na wataalamu wa JKCI wameweza kuchangi Sh bilioni 4.5 toka walipoanza matibabu haya miaka mitano sasa.

Amesema kwasasa wataalamu hao wametoa matibabu ya Sh milioni 700 kwa watoto hao 30 waliofanyiwa upasuaji wa moyo.

Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Yahya Okeish aliwashukuru madkatari na timu yote kutoka kituo cha King Salman na madkatari wa JKCI kwa kufanikisha matibabu ya watoto hao.

SOMA : NIC waja na Bima ya Maisha

“Ninaona heshima kushiriki nanyi kuhitimisha kambi hii ya matibabu ya moyo  huu ni ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia na tunapata faida hasa kwa watu tunafurahi naamini kuwaona tena wakitembelea Tanzania tena.

Naye mmoja wa wazazi Ester Shauri kutoka Mkoa wa Mbeya amesema haikuwa rahisi mtoto wake kupata matibabu  kwasababu shida ilikuwa kubwa ameshukuru kwa kambi hiyo na kufanya upasuaji kwa watoto.

“Mwanzo mtoto alikuwa anachoka mapema ila sikuweza kugundua kwasababu alikuwa haumwi mara kwa mara sikujua ni shida lubwa nimekuja kugundua mwezi wa sita mwaka huu.

Ameongeza “Nilivyompeleka hospitali walisema anashida kwenye moyo kwa hospitali ndogo hawakuona tatizo ndo wakasema nimpeleke hospitali kubwa.

Habari Zifananazo

Back to top button