TIMU ya mpira wa miguu ya watumishi mashabiki wa Yanga katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao Simba kwenye bonanza la kumbukizi ya miaka 25 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Kwa upande wa mpira wa mikono timu ya Yanga pia imeibuka na ushindi wa goli 22 huku Simba wakijipatia 19, bonanza ambalo limefanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo.
SOMA: Waendesha baiskeli 200 kumuenzi Nyerere
Licha ya bonanza, pia kumefanyika matembezi ya amani lengo ni kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Michezo mingine iliyofanyika ni kukimbiza kuku, kuvuta kamba ambapo yote timu ya Yanga ilibuka na ushindi dhidi ya mpinzani wake Simba.
Mkurugenzi wa manipaa hiyo, Hassan Nyange amesema matukio hayo yote yameyofanywa katika siku hiyo ni kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu uchaguzi huo.
‘’Lakini pia ikiwa sambamba na wiki hii ya vijana na kukumbushwa pia kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi ni afya na itakuwa utaratibu sasa wa manispaa tunakwenda kuanzisha timu itakayofanya joging kila Jumamosi,’’amesema Nyange