DAR ES SALAAM :ZAIDI ya waendesha baiskeli 200 kutoka nchi mbalimbali kushiriki msafara wa Twende Butiama kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka kampuni ya simu ya Vodacom, Zuweina Farah amesema Kampuni ya Vodacom na taasisi zake zinalengo moja kwa jamii ikiwa ni Elimu bora , afya na kuwawezesha wajasiriamali wadogo kuwainua kiuchumi.
Amesema katika mpango wa miaka mitano ijayo wamelenga kuzisaidia shule katika mikoa 12 hadi14.
DAR ES SALAAM :ZAIDI ya waendesha baiskeli 200 kutoka nchi mbalimbali kushiriki msafara wa Twende Butiama kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka kampuni ya simu ya Vodacom, Zuweina Farah amesema Kampuni ya Vodacom na taasisi zake zinalengo moja kwa jamii ikiwa ni Elimu bora , afya na kuwawezesha wajasiriamali wadogo kuwainua kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa Twende Butiama Gabriel Landa amesema msafara huo utamuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo kwa kupambana na maadui wa maendeleo ambao ni ujinga, umaskini na maradhi
Amesema msafara huo uutashirikisha watanzania wengine kuadhimisha kumbukizi ya kifo cha miaka 25 cha Baba wa Taifa tangu alipofariki
SOMA: Taasisi yaenzi miaka 101 ya Nyerere
Msafara huu utahusisha kilomita 1,846 kutokea Dar es salaam hadi Butiama huku wakitegemea kupata washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania nan chi zingine kama Zimbabwe,Afrika Kusini, Namibia lengo kuwaleta pamoja watanzania na waafrika katika kuishi maono ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.